TUFAHAMU

Gospelclinic.net ni mtandao maalum uliobeba nia ya uinjilishaji. Kutoa habari mbalimbali za kijamii, mafundisho ya neno la Mungu, ujasiriamali, mziki na mengine mengi.

***

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema”. 2Tim3:16-17

Facebook

Tafadhali, unaweza kutembelea ukurasa wetu wa facebook kwa habari na taarifa mbalimbali

Instagram

Tafadhali, unaweza kutembelea ukurasa wetu wa Instagram kwa habari na taarifa mbalimbali.

Youtube

Tafadhali, unaweza kutembelea chaneli yetu ya Youtube, kwa mafundisho ya neno la Mungu.

Baraka!

Mnamo mwaka 2010 maono ya Gospel Clinic yalizaliwa. Yakiwa yamelenga kuinjilisha kwa njia ya mtandao yaani kufikisha habari zote njema zinazohusu afya ya mwili na roho pamoja na kupata taarifa mbalimbali zinazotuzunguka katika maisha ya kila siku zitakazoweza kututafakarisha kiroho.

Maono haya si madogo kwetu, kutokana na ukubwa na uzito wake, gospel clinic “team” inategemea sana ushirikiano wa kila mtoto wa Mungu anayesoma ujumbe huu saa hii, kushiriki nasi katika kuitangaza habari njema, kwa njia ya kushirikisha wengine masomo yanayopatikana katika tovuti hii. Mchango wa maombi ni muhimu sana kwetu, ili kazi hii iwafikie watu wengi zaidi wapate kujifunza na kuokolewa. Mungu akubariki sana.