Wajasiriamali wengi wanajihusisha na mitandao ya kijamii lakini hawana lengo la moja kwa moja la kutumia nafasi hiyo kama fursa ya shughuli wanazozifanya. Wengi wanaitumia kama sehemu ya “ku-refresh akili” tu. Uwezo wa kuona mbali ni sifa ya mjasiriamali yeyote mwenye nia dhabiti ya kufanikiwa. Weka nia ya kuifanya biashara yako ifahamike zaidi na kuongelewa zaidi midomoni mwa watu. Ona milango ikifunguka kupitia mitandao, fahamu kwamba mitandao ya kijamii ndio sehemu pekee ambayo unaweza kufanya biashara yako kwa uhuru zaidi na kwa watu wa eneo kubwa kama sio dunia nzima.   2. TENGENEZA BRAND. Tengeneza mazingira ambayo watumiaji wa mitandao watakutambua kwa urahisi. Kuwa na logo yako itakayoweza kukutambulisha au kuitambulisha bidhaa au biashara yako popote. Tafuta jina zuri na rahisi, kisha anza kulitumia katika bidhaa zako au katika kila post unayoipeleka mtandaoni. Tengeneza labels zenye mvuto ambazo mteja akiona itaweza kumvutia. Kumbuka thamani ya bidhaa huongezeka kwa kadiri utakavyoweza kuiongezea thamani hiyo bidhaa. Sahani ya chakula cha tsh 3,000 inaweza kuuzwa tsh 5,000 kama tu umekiweka katika kifungashio kizuri kitakachoongeza muonekano wa “Package” ya chakula. Usipende kubadilibadili logo au jina la biashara mara kwa mara hii ina punguza umakini kwa wateja au kwa wale wanaofuatilia kazi yako. Tengeneza brand yako, kuza brand, linda brand.   3. TENGENEZA MTANDAO (NETWORK) Ingia rasmi kwenye ulimwengu wa mtandao, jiunge na groups mbalimbali zinazoendana na yale unayoyafanya, tengeneza marafiki wapya wenye mtazamo chanya. Tengeneza pages za mtandaoni ambazo zitaibeba biashara yako. Angalia ni mtandao upi utaweza kuutumia vizuri zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi, unaweza kuwa mtandao zaidi ya mmoja. Mahusiano yako na mteja ni kitu muhimu sana. Jenga tabia ya kuwasiliana moja kwa moja kwa kuongea na mteja, zuia maongezi ya meseji zaidi kwani wakati mwingine huwasilisha hisia za tofauti na kile ulichokidhamiria.   4. WAAMINISHE WAFUATILIAJI WA KAZI ZAKO. Jali sana mpangilio wa picha zako mtandaoni, ubora wa picha na maudhui ya picha yasadifu kile unachokifanya. Hakikisha unafuatilia “account” yako mara kwa mara na ku-post picha pia… hii inafanya account kuwa “active”. Jibu maswali ya wateja kwa wakati bila kuchelewa kwani wateja wa mtandaoni wengi ni wapitaji tu na huvutiwa na kitu pale wanapokiona tu.   5. JIFUNZE KITU KIPYA KILA SIKU Unafanya biashara ya aina gani? Jifunze zaidi, usiache siku ipite hujagundua mbinu mpya ya kuikuza biashara yako. Fuatilia wanaofanya biashara kama yako wanafanyaje. Tumia mitandao kama Youtube, whatsapp kuuliza na kutazama mafundisho kila siku. Tenga muda walau saa moja kujifunza. Usichoke kama mtu unaweza kumfikia basi nenda mtembelee ukajifunze kitu. Pamoja na hayo, jifunze lugha za mtandaoni kama hashtags(#), tags, location n.k hivi pia ni muhimu kwa matangazo ya mtandaoni. Mfano: unapotumia hashtag kwenye neno hand bag… utaliandika #handbag bila kuacha nafasi. Hashtags zinamsaidia hasa mteja au mtumiaji mtandao anapotafuta kitu husika, kwahiyo kama mtafutaji akiandika #handbag atakuta post zako na za watu wengine duniani waliotumia hiyo hashtag. Pia matumizi ya “location” (mahali ulipo wakati unapost) ni nzuri zaidi kutumia eneo la ofisi yako kama njia ya kuitangaza ofisi ilipo.   6. “PROMOTE” BIASHARA. Hakikisha kazi zako unazoweka kwenye mitandao ya kijamii zinawafikia watu wengi. Zingatia kutuma picha nzuri, lipia gharama za promo za mtandao ili kuipa nafasi account yako kuonekana na watu wengi zaidi. Jitahidi pia kuweka offer kama sehemu ya kujitangaza.
Previous post

UFAHAMU NA MAARIFA

Next post

"SHETANI NI MUONGO NA BABA WA HUO"

Rodgers Mathew

Rodgers Mathew

Gospel Clinic Website Developer.

No Comment

Leave a Reply