SHETANI NI MUONGO NA BABA WA HUO.

 1. Shetani ni muongo na baba wa huo. “Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.” Yoh 8:44c
 2. Shetani hakubali siri zake zitoke au zijulikane.
 3. Huzuia watumishi wazuri wasichomoze.
 • Huwagombanisha
 • Huwaibulia skendo za kuvunja moyo
 • Huwatia hali ngumu ya kiuchumi
 • Huwainulia tuhuma za uongo n.k
 1. Hatoi nafasi wanaozijua siri zake wazitoe. (Yuko tayari kuutoa uhai wao)
 2. Anatumia mlango wa hisia, mfano uchungu, hasira.. kurudia makazi yake. “Mara nyingi huujua udhaifu wa mhusika”.
 3. Kwa wale waliofanyika kuwa “kisiki” (Mapepo yasiyotaka kutoka).
 • Inapasa kumwombea toba pamoja na kuhakikisha yeye binafsi amefanya toba ya kweli.
 • Kufahamu mambo muhimu yanayomhusu hasa ya maisha yake ya nyuma.
 • Kumpa ushauri wa kiroho kwa upendo kwa lengo la kuirejesha nafsi iliyoharibiwa na kuchoshwa na adui.
 • Kumpatia utajiri na siri za Neno la Mungu. Mfundishe waziwazi tabia au hali zitakazomfanya asiweze kuwa huru iwapo hataamua kuziacha mfano Uoga, hasira, uchungu, kutosamehe n.k
 • Mfundishe mbinu za kupambana kwa njia ya maombi.
 1. Hakuna mtumishi aliye salama.
 2. Shetani akimtaka mtu hutumia mbinu mbalimbali, kuwa makini sana mtumishi wa Mungu. Jitahidi kuwa hai rohoni, milango ya fahamu ya rohoni iwe “active” wakati wote.
 3. Usiipuuzie kauli yoyote ya shetani. Maneno machafu dhidi yako si salama, “jikung’ute kwa njia ya maombi kupitia damu ya Yesu Kristo”.
 4. Ibilisi hana huruma. Hana urafiki na mwanadamu, kwa anayemtumikia na asiyemtumikia.
 5. Anatengeneza chuki.
 6. Anatengeneza magonjwa.
 7. Ni chanzo cha tabia zote chafu; umalaya, ulevi, uchawi, n.k
 8. Wapo watu waliotunukiwa roho za kijini na vyeo vya kipepo ili watawale katika roho na katika mwili.
 9. Anaweza kumfanya mtu ajikatae ajione hafai, hapendwi, hana thamani.
 10. Maombi yenye bidii ni silaha bora ya kuziangusha ngome ngumu za ibilisi.
 11. Watu waliodhaifu kiroho huweza kukamatwa na adui au kutumikishwa kwa kujua au kwa kutokujua.
 12. Mtu anaweza kumpenda au kumtamani mtu pasi kutumia ufahamu wake.
 13. Ibilisi anaweza kuvaa sura ya mtu ili kufanikisha hila zake. Maombezi ya walioathirika na matendo ya kingono na umalaya hutumiwa sana na mbinu aina hii. Ibilisi hutumia sura za watumishi kuvuruga imani ya mhudumiwa.
 14. Mapepo yana vitengo mbalimbali kwa ajili ya kuratibu tabia zote mbaya za mtu.
 15. Shetani hachagui eneo la mapambano. “shina la uchungu ni ngome ya mapepo”. “mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.” Ebrania 12:15.
 16. Shetani huweza kumpa mtu ugonjwa na kuuondoa akiamua. Shetani hutenda kazi ndani ya wigo wake wa uongo.
 17. Shetani ana uwezo wa kumtokea mtu kama malaika wa nuru. “Wala si ajabu. Maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.” 2Kor 11:14
 18. Huwezi kumteta wakala wa shetani hata kama amelala. Mapepo hayalali. Ulimwengu wa roho upo macho muda wote.
Previous post

NJIA 6 ZA KUKUZA BIASHARA YAKO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII

Next post

25 TIPS ON HOW I CAN READ MY BIBLE.

Rodgers Mathew

Rodgers Mathew

Gospel Clinic Website Developer.

No Comment

Leave a Reply