Mwanzo 39:4-22

Yusufu alikuwa mtu mwenye MAONO aliye jitambua na alijua wapi anakwenda, ndiyo maana baada ya mke wake Potifa kumtamani alikataa nakusema ” siwezi kutenda ubaya huu, nimkosee Mungu “

Yusufu alijua akijichanganya ndoto zake zitaishia palepale.

Kuwa mwaminifu kuna kufungulia milango mingi sana, maana uaminifu huwa hauna hasara hata siku moja. Watu wanaweza kukuona haufai unaziba ulaji wao kazini, lakini fyekeo likija nakwambia utabaki wataondoka…

Wewe kuwa mwaminifu hata kama itakugharimu kufukuzwa kazi, wakati utakuja watajua kuwa wewe ndiye unayestahili kupewa nafasi kuu zaidi. Uaminifu ni gharama maana wakati mwingine hugharimu hata maisha yako.

Ndiyo maana neno linasema uwe mwaminifu hata kufa, yani uwe tayari hata kufa lakini usiache kuwa mwaminifu, na Mungu akisha uona uaminifu wako atakutetea kama alivyo fanya kwa Yusufu maana mwenye MAONO hafi nje ya mpango wa Mungu.

Watu wengi integrity (Uadilifu) imekuwa ni shida sana, akipewa nafasi tu basi, ni mipango ya wizi kwenda mbele, nikushauri kitu, hakuna mwizi asiye lipwa hapa hapa duniani, hata kama usipo kamatika, Mungu atakuadhibu kwa njia ya magonjwa, mipango yako binafsi ku fail n.k

Hakuna hasara ya kuwa mwaminifu, na katika MAONO yako ya kufika mbali katika mipango yako, usijichanganye.. hutafika,¬†adui mkubwa wa VISION kwa mwamini ni DHAMBI… Yusufu alijua akijiloga tu, mwisho wake ulikuwa pale.. lakini uaminifu wake ulimpa kibali kila alipo kwenda, hadi gerezani alipata kibali kwa mkuu wa gereza Mwanzo 39:21

Uaminifu huleta kibali, kumbuka kibali ni zaidi ya umaarufu. Watu wengi hutamani kuwa maarufu na kusahau kuwa kibali ni muhimu sana kuliko umaarufu, na umaarufu unaweza kuununua, kwa promotion n.k lakini kibali hutoka kwa Mungu.

Na kibali ndicho hukufanya ubaki nafasi ya juu kwa muda mrefu.

Tabia njema na kujizuia ni vitu vya msingi katika kukufanya uwe mwaminifu na hayo yote huzaa Uadilifu (Integrity). Huwezi kwenda kokote wala kufanikiwa kwa lolote kama wewe si mwadilifu utafika mahali tu utakwama.

Uaminifu/uadilifu hufungua milango ya chuma ili wewe upite, hukupa heshima mbele za watu na hata ukiwa na shida uaminifu na uadilifu wako husimama mbele yako kukutetea na kukusaidia.

Kama huna pesa, huna elimu, wala huna connection yoyote, mtaji pekee uliobaki nao ni UAMINIFU kwa kile kitakacho kuja mikono mwako. Dunia inatafuta watu waaminifu na waadilifu lakini siku hizi hawapatikani ki rahisi, anza wewe na utaona mabadiliko katika kila ulifanyalo.

Kwa msaada na ushauri wasiliana nasi:
Mwl Kabenda Balete
0657606556
Dar es Salaam.

Previous post

UPENDO

Next post

USIPENDE PESA ZA HARAKA.

Rodgers Mathew

Rodgers Mathew

Gospel Clinic Website Developer.

2 Comments

  1. Pery
    June 18, 2019 at 6:48 pm — Reply

    Nimebarikiwa sana na hili somo, Mungu awabariki…

    • June 19, 2019 at 7:06 pm — Reply

      Asante! endelea kufurahia huduma zetu. Mungu akubariki…

Leave a Reply