Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.

Mithali 13:11

Mpendwa nakusalimu, natumai, u mzima wa afya…

Leo tutafakari neno hili pamoja, ambalo Sulemani alikuwa akimwambia mtu anaye penda pesa au mali ya haraka haraka.

Katika kipindi changu cha ujasiliamali, nimekutana na vijana wengi wanao penda kufanikiwa haraka haraka.

Niseme kitu kimoja tu kuwa, mali inayo kuja kwako haraka, huondoka haraka kwako kwa sifa kuu moja tu, ni kwamba inakuta kichwani kwako huna mipango yoyote ile ya kuzalisha.

Kumbuka pesa haipendi kutumiwa, wala kutunzwa, pesa inapenda kuzalishwa, ikija kwako ukawa na mawazo hayo mawili, huondoka haraka na kwenda kwa mtu anaye weza kuzizalisha.

Pesa haiwezi kukaa kwa mtu maskini wa mawazo, maana umaskini si kukosa pesa au mali ingekuwa hivyo mtu anayepata mali au pesa kwa haraka angefuta umaskini wake.

Lakini bahati mbaya ni kwamba ukipata pesa haraka au mali ya aina yoyote, na ukiwa huna mawazo ya kuzalisha, mali au pesa hizo huondoka na kukuacha maskini zaidi ya mwanzo kabla hujazipata hizo pesa.

Maana pesa ikija kwako na ikakuta, huna mawazo ya kuzalisha utakacho fanya ni kuzitumia na kununua vitu visivyo dumu, itakutengenezea mazingira ya maisha ya juu kuliko mwanzo kabla hujazipata, utaanza kuishi maisha kana kwamba wewe umesha toka na kumbe zikiondoka hukuacha juu juu, na huanguka na kusagika kabisa.

Usipende kupata pesa inayokuja kwako bila kuiwekea misingi ya kuizalisha, pesa inakaa kwako kwa sababu una mipango thabiti ya kuizalisha vizazi na vizazi, mtu yeyote mwenye uchoyo wa kutaka achume mali azile peke yake na wengine wajijue au watafute mali zao akifa huyo hufa maskini wakutupwa.

Kuchuma kidogo kidogo haimaanishi, kuuza vitu vidogo vidogo la hasha, ina maanisha mali idumuyo huwekewa misingi imara ili ikue kidogo kidogo, kwa sababu ikija haraka hutokuwa na stamina ya kuhimili kishindo chake, lakini mali unayo kua nayo inakupa kujifunza changamoto na kuzitatua.

Pesa nyingi, changamoto nyingi na pesa kidogo changamoto kidogo, ukijenga biashara yako kuanzia chini na kukua nayo, hakuna kitu kitakacho kushinda ku manage, lakini ghafla ukiambiwa wewe ni CEO wa kampuni yenye mtaji wa mfano bilion moja, nakwambia hakika maamzi yako ya haraka haraka yataifanya kampuni ife au board ya wakurugenzi itakufukuza.

Lazima ujue kuwa Mungu hatoi pesa, anakupa kujua jinsi ya kujenga uchumi imara unao kua, ndiyo maana neno linasema. Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. 1 Timotheo 6:9

Mpendwa wangu usipende pesa au mali; pesa hujileta zenyewe pale unapo kuwa umeweza kuweka suluhu ya matatizo katika jamii, Pastor Kuria (Kenya) alisema, fedha ni zawadi baada ya kutatua matatizo ya watu.

The moment unapenda maisha mazuri na ya kifahari bila kujua misingi ya kupata pesa hiyo basi wewe hudondokea kwenye kundi la wanaotaka uharibifu wa maisha yao.

Tunahitaji pesa ndiyo, lakini ukiihitaji bila kuwa na huduma yoyote unayotoa kwa jamii ili pesa zije, basi wewe unataka kisu cha kukuua mwenyewe. Usipende pesa kiasi kwamba unatamani uibe, kuna watu wanahitaji pesa hadi wanatetemeka wakiona wenzao wanavyo tembelea magari mazuri, nyumba nzuri n.k.

Hata kama ungepewa mamilioni ya pesa kama kichwani kwako ni kweupe zitaondoka kwa pupa kama neno lilivyo sema.

Maskini anasifa kuu mbili kama nilivyosema hapo juu, 1. Anawaza Kutumia pesa tu 2. Zikimshinda kumaliza anazitunza ili kesho azishugulikie tena hadi ziishe

Mimi nakusihi tu, usipende pesa, penda kuweka misingi ya kuzitega pesa zitajileta na utaishi maisha mazuri unayo yahitaji.

Ila kumbuka tu pesa hufuata mtu mwenye VISION ( MAONO) ili zije kufanya kazi na siyo kutumbuliwa tu.

Hakika nakwambia….

Wasiliana nasi:
Mwl Kabenda Balete
0657606556
Dar es Salaam.

Previous post

UAMINIFU UNALIPA

Next post

The Good Person Test.

Rodgers Mathew

Rodgers Mathew

Gospel Clinic Website Developer.

No Comment

Leave a Reply